News
Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe Hamis Mwinjuma ameliagiza Baraza la Sanaa la Taifa “BASATA” na Bodi ya Filamu Tanzania kushirikiana na mashirikisho, Vyama vya Wasanii na taasisi za kifedha kuandaa mpango mahususi utakaowezesha wasanii watakaokuwa tayari wawe na bima za Afya na akiba za uzeeni.
Mhe Mwinjuma ameyasema hayo Agosti 2, 2024 jijini Dar es salaam wakati akitoa neno kwa wasanii katika mkutano wa wasanii wa utoaji wa elimu ya fedha kwa wasanii ‘Sanaa Pesa Summit’
“Huwa naumia sana napoona msanii akiomba kuchangiwa fedha hasa wakati wa matatizo ya ugonjwa kutokana na kukosa bima ya afya au pale wasanii tunapokuwa tumeishiwa nguvu kutokana na uzee na kugeuka kuwa omba omba kutokana na kukosekana kwa mfumo mzuri wa kujiwekea akiba uzeeni. Hili kwa kiasi kikubwa linachangiwa na ukosefu wa elimu muhimu kama iliyotolewa leo”
“Naomba niweke wazi kuwa nafungua milango kwa wadau kutoka katika sekta ya fedha washirikiane na Wizara yetu kuhakisha wasanii wanakuwa na elimu ya kutosha kuhusu masuala ya kifedha pia huduma rafiki zitakazomvutia msanii kujiunga ili tuweze kujenga kesho yetu iliyo bora