News

Posted On:: Sep, 05 2024
News Images

Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Gerson Msigwa Septemba 4, 2024 amekagua ujenzi wa jengo la ofisi za wizara hiyo ambalo liko katika hatua za mwisho za ukamilishwaji katika mji wa Serikali, Mtumba Jijini Dodoma huku akiwa ameongozana na Naibu Katibu Mkuu, Methusela Ntonda pamoja na menejimenti ya wizara hiyo ambapo kwa pamoja wameridhishwa na hatua ya ujenzi wa jengo hilo.

Katibu Mkuu Msigwa amesema kasi ya mkandarasi inaridhisha akieleza kuwa ujenzi huo umefikia zaidi ya asilimia 87 akibainisha kuwa kazi zinazoendelea kufanyika sasa ni ufungaji wa vioo,madirisha, milango na kupaka rangi.

Aidha, Katibu Mkuu Gerson Msigwa amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuhakikisha Wizara inapata majengo ambayo yatasaidia kutatua changamoto mbalimbali ikiwemo ya watumishi kufanya kazi katika maeneo tofauti pamoja na baadhi ya taasisi kufanya kazi katika majengo ya kupanga.