News

Posted On:: Sep, 09 2024
News Images

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro. amewaagiza viongozi wa klabu za Jonging nchini, kuandaa kalenda maalumu ya matukio yao ili kurahisisha utaratibu kwa wananchi kushiriki matukio hayo ambayo yanaimarisha afya na kudumisha uhusiano.

Ametoa maagizo hayo Agosti 8, 2024 Wilayani Muheza mkaoni Tanga, wakati aliposhiriki tamasha la kuadhimisha miaka 10 ya Muheza Jogging and Sports Club tangu kuanzishwa kwake.

Akizungumza baada ya kushiriki mbio za tamasha hilo, Mhe.Ndumbaro amewapongeza waandaaji wa tamasha kwa kuunga mkono utekelezaji wa maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ya kufanya mazoezi ili kuimarisha afya na kujikinga na magonjwa yasiyoambikiza.

Awali akizungumza kwa njia ya simu kutoka Jiji la Yamasoukro Nchini Ivory coast ambapo anaongoza msafara wa timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu (Taifa Stars) katika mchezo wa kufuzu AFCON 2025 dhidi ya Guinea , Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo na Mbunge wa Jimbo hilo Mhe. Hamis Mwinjuma amewataka wana Muheza kudumisha mazoezi ili kulinda afya zao.

Jumla ya klabu za Joging 84 zimeshiriki katika tamasha hilo, lililo sindikizwa na kaulimbiu ya "Serikali za Mitaa Sauti ya Wananchi, Jitokeze Kushiriki Uchaguzi".